mafunuo

Jana Yesu alinikutanisha na binti mmoja katika ulimwengu wa roho kutoka Singida, na nilikuwa nikimuuliza juu ya mambo mbali mbali kuhusu maisha yake.
Ni binti aliye okoka, yuko kidato cha nne, lakini anapitia wakati mgumu kiroho na kitaaluma. Wanaume wa mtaani walimrubuni kuwa wanampenda na wanaishia kumtumia. Lakini pia kuna baadhi ya vijana waliookoka wanao msumbua. Inafika wakati hata watu wazima katika jamii wanashindwa kutoa msaada unao takiwa kwa wengi wa mabinti hawa. Haya yote ni kwasababu hawa mabinti hawaja lelewa vizuri katika maarifa na nguvu ya upendo wa Mungu katika nyanja mbalimbali za maisha yao. Kwa kweli tuliongea vitu vingi sana.

Naomba uungane nami kumwombea binti huyu na mabinti wengine kama hawa waliookoka, hasa wa shule za sekondari. Hawa watu wanahitaji kujua zaidi upendo wa Mungu, kuishi na kukua katika nguvu ya upendo wake kupitia neno lake.
Mungu akubariki!

Comments

Popular posts from this blog

THE TRAINING MINISTRY OF THE SPIRIT OF LOVE FUNCTIONS BY REVELATION

LEARNING AND PRACTISING

POSITIONING YOURSELF FOR THE UNLIMITTING OF PEOPLE'S SPIRITUAL SENSES AND SPIRITUAL SENSATIONS